Hii ilitokea na haikuwahi kuandikwa, siku moja tu
baada ya Simba kumtupia virago Kocha Zdravko Logarusic, akaibuka kocha
mwingine.
Kocha huyo ni shabiki wa Simba aliyekuwa amezoea
kwenda mazoezini na kuona Loga raia wa Croatia alivyokuwa anafanya mazoezi
yake.
Taarifa za kutimuliwa kwake zilianza kusikika
jioni na siku iliyofuata.
Hivyo inaonekana shabiki huyo alijiandaa mapema
akijua asingemuona Loga, hivyo angefanya kazi hiyo yeye bila ya ruhusa ya
uongozi.
Jamaa huyo, inaonekana alikuwa amepiga ‘maji’ ili
kuongeza ujuzi na alipofika kwenye Uwanja wa Ununio, kweli hakumuona Loga
badala yake Kocha Msaidizi, Selemani tu. Jamaa huyo akaamua kuchukua nafasi ya
ukocha mkuu na kuanza kutoa maelekezo.
Raha ilikuwa zaidi pale jamaa alipokuwa akifanya
matendo kama yake ya Loga, halafu usisahau jamaa naye ana kipara kama Loga,
basi watu walikua wanaangua vicheko. Hata wachezaji wakati mwingine walishindwa
kujizuia.
0 COMMENTS:
Post a Comment