November 24, 2014


Kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kiwhelo ‘Julio’ amesema kesho anakutana na Rais wa Simba, Evans Elieza Aveva ili kumueleza uamuzi wake wa kuwataka wachezaji watano kutoka Simba.

Julio amewataja baadhi ya anaowahitaji Simba kuwa Said Nassor ‘Chollo’, Abdallah Seseme, Uhuru Selemani na wengine wawili.

“Nataka kuimarisha kikosi changu kwenye diridha dogo lakini haina maana wachezaji wangu nilionao hawafai.
“Simba kuna wachezaji ninawataka, nitakutana na Aveva na kupata nafasi hiyo ya kumueleza ninachohitaji,” alisema.


Mwadui FC ya mkoani Shinyanga imekuwa na mwenendo mzuri kwenye Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara na iko kwenye kundi la timu zenye matumaini ya kucheza Ligi Kuu Bara.

Julio amewahi kuwa kocha wa Simba kwa vipindi tofauti, pia amewahi kuichezea timu hiyo akiwa beki tegemeo wa kati hadi kufikia kupewa jina la 'Mrema'.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic