Luis
Suarez alifunga bao na kuisaidia Uruguay kupata sare ya mabao 3-3 dhidi ya Costa
Rica katika mechi iliyopigwa jijini Montevideo.
Lakini
baadaye ikapigwa mikwaju ya penalti na Uruguay wakalala kwa 7-6.
Kivutio
zaidi kilikuwa pale Suarez alipochaniwa jezi yake na kipande kuanguka uwanjani.
Suarez
alichaniwa jezi hiyo wakati akipambana na Giancarlo Gonzales wa Costa Rica.
Mechi
hiyo ya kirafiki ilikuwa na ushindani mkali kuliko hata ile ya mashindano.
Leo
asubuhi, magazeti na vyombo vingi vya habari vilizungumza kuhusiana na kipande
hicho cha jezi badala ya kipigo cha timu ya taifa ilichokipata kutoka kwa
wageni.
0 COMMENTS:
Post a Comment