November 27, 2014


Kocha wa zamani wa Yanga, Hans van der Pluijm ameondoka kwake Ghana kurejea Uholanzi ili awahi kushuhudia mechi ya Ligi Kuu Uholanzi.



Pluijm aliyeinoa Yanga kwa muda mfupi na kuwa tishio, amesema alikuwa na mpango wa kurejea kwao Uholanzi kuiona familia yake, lakini ameamua kwenda mapema awahi kuinoa mechi kati ya PSV dhidi ya Feyernood.

"Ni mechi nzuri kuona, kuna mambo mengi sana, pamoja na burudani lakini kujifunza.
"Nitaondoka mapema kesho ili niwahi kwenda kuiona," alisema.

Pluijm aliiwezesha Yanga kuifunga Al Ahly jijini Dar kwa mara ya kwanza, lakini Yanga ikatolewa kwa mikwaju ya penalti mjini Alexandria nchini Misri.

Pluijm anaishi nchini Ghana na aliiacha Yanga na kwenda Saudi Arabia katika klabu ya Al Shaola, lakini hakudumu baada ya kutoelewana na uongozi, akarejea tena Ghana.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic