Mshambuliaji Mnigeria, Emeh Godwill Izuchukwu yuko njiani kurejea
Simba kama ambavyo blogu hii ilivyoandika wiki iliyopita.
Taarifa za uhakika zimeeleza, suala la kodi
kubwa ya nyumba na gharama za maisha ya nchini Norway, zimechangia Mnigeria
huyo kurejea Simba.
“Ni kweli, analipwa vizuri angalau, lakini kodi
ya nyumba na maisha yako juu sana Norway, hivyo hapati chochote mwisho wa
mwaka.
“Nimezungumza na viongozi wa Simba, wamesema
wanalijadili lakini kuna asilimia kubwa za kurudi,” kilieleza chanzo.
Izuchukwu
sasa anakipiga katika timu ya daraja la pili ya Elverum FC ya nchini Norway.
0 COMMENTS:
Post a Comment