November 25, 2014


Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Thomas Mashali anatarajiwa kupanda ulingoni Januari Mosi, mwakani katika pambano la kirafiki litakalomkutanisha na Abdallah Pazi maarufu kwa jina la ‘Dulla Mbabe’ wa jijini Dar es Salaam.

Wiki mbili zilizopita, Mashali alimchakaza kwa KO mbaya bondia kutoka nchini Kenya.

Mashali amesema kuwa pambano hilo linatarajiwa kuwa la raundi 8, litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Friends Corner, Kagera jijini Dar.

“Sasa hivi nimehamua kuwa mjasiliamali kwa kuandaa mapambano yangu mwenyewe. Pia kwa mabondia wengine kwa kuanza na hili nitakalopigana na Dula Mbabe Januari Mosi, mwakani kwenye Ukumbi wa Friends Corner.

“Hivi sasa ninaendelea na mazoezi ya nguvu kuhakikisha ninakuwa fiti kwa ajili ya pambano hilo, ninajua mpinzani wangu yupo vizuri, hivyo ninajiandaa vyema ili nimpige Dulla Mbabe,”alisema Mashali.
Mashali ni kati ya mabondia bora nchini ambao wamekuwa wakifanya vizuri ndani na nje ya nchi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic