Kiungo
mshambuliaji mwenye kasi wa Yanga, Simon Msuva amefunguka na kuwaambia Simba
kwamba aingependa waendelee kumzungumzia.
Msuva amesema
kama Simba wanamhitaji, vizuri wakafuata utaratibu na kuzungumza na Yanga
kuliko kuendelea kumzungumzia kwa kuwa wanamchanganya.
Msuva kutoka
mkoani Iringa amesema mkataba wake wa mwaka miaka miwili na Yanga ambao umebaki
mwaka mmoja na nusu, unamfanya ahamishie mawazo yake yote Jangwani.
“Kwa kweli
niko ndani ya mkataba, hivyo nawaomba Simba wazungumze na Yanga kuliko
kuendelea kunizungumzia.
Vitu
vinavyofuata utaratibu ndiyo bora, nisingependa kuona wanaendelea kunizungumzia
kila wakati, inanichanganya kwa kweli.
“Nauheshimu
mkataba wangu na matumaini yangu makubwa ni Yanga kwa sasa,” alisema Msuva.
Tayari Simba
imesema itapeleka barua Yanga kumtaka Msuva kwa dau la Sh 500,000, lakini Yanga
wamekuwa wakisisitiza, hakuna barua yoyote kutoka Simba na badala yake wamekuwa
wakisikia kwenye vyombo vya habari tu.
0 COMMENTS:
Post a Comment