MKURUGENZI WA MASHINDANO WA TFF, BONIFACE WAMBURA. |
Michuano
ya Ligi Daraja la Pili (SDL) msimu huu iliyokuwa ianze kutimua vumbi Novemba 22
mwaka huu kwa mechi kumi katika viwanja vitano tofauti imesogezwa mbele hadi
Desemba 6 mwaka huu.
Mechi
hizo zimesogezwa ili kutoa fursa ya kukamilisha maandalizi mbalimbali ya ligi
hiyo inayoshirikisha timu 24 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara.
Mikoa
yenye timu katika ligi hiyo ni Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Katavi,
Kigoma, Lindi, Mara, Mbeya, Morogoro, Mwanza, Njombe, Pwani, Rukwa, Ruvuma,
Shinyanga, Singida na Tabora
0 COMMENTS:
Post a Comment