Yanga imefanikiwa kumsainisha mshambiliaji Danny Mrwanda wa Polisi
Morogoro.
Mrwanda amesaini mkataba wa kuichezea Yanga
kwa mwaka mmoja ikiwa ni siku chache baada ya kufanya mazungumzo na Simba.
Simba ndiyo ilikuwa imsajili Mrwanda, lakini
siku moja kabla ya kumsainisha ikaahirisha kwa madai hakueleza ukweli kwamba
mkataba wake na Polisi unamruhusu kucheza nje ya nchi na kama ni nchini, basi
lazima Polisi ilipwe.
Leo Yanga imefanikiwa kumsainisha
mshambuliaji huyo ambaye imeelezwa uzoefu wake umekuwa ni sehemu ya sababu.
0 COMMENTS:
Post a Comment