SIMON SSERUNKUMA |
Mshambuliaji wa Simba, Amissi Tambwe tayari mguu mmoja uko nje ya klabu ya Simba.
Lakini mtu ambaye anaweza kuamua abaki au aondoke ni mmoja tu, Simon Sserunkuma.
Sserunkuma ni mdogo wa Danny Sserunkuma, mshambuliaji mwingine Mganda wa Simba ambaye ndiyo atakuwa anaichezea timu yake kwa mara ya kwanza katika mechi dhidi ya Yanga.
Simba itaitumia mechi hiyo kumuangalia Sserunkuma mdogo ambaye anakipiga Express.
Kama atafanya vizuri leo na Simba ikachukua uamuzi wa kumsajili, basi Tambwe ndiyo byebye.
Ila kama Sserunkuma atachemsha, basi Simba ina kila sababu ya kuamua Mrundi huyo mfungaji bora msimu uliopita, aendelee kubaki.
0 COMMENTS:
Post a Comment