December 15, 2014


Ulizoea kumuona akirundikiwa lundo la kadi, sasa unajidanganya, beki Pepe ni mtu mwingine.
Ukipenda muite “Mr Clean”, kwa kuwa hadi sasa amesababisha faulo tano tu.

Achana na faulo hizo chache, Pepe ambaye ndiye beki tegemeo wa Real Madrid akiunda ukuta na Sergio Ramos, hana hata kadi moja ya njano.

Hadi sasa , Pepe ndiye beki wa kati mwenye kadi chache zaidi kwa wale wanaozichezea timu zao katika La Liga.

Mreno huyo mwenye miaka 31, ameonyesha mabadiliko makubwa na kuwashangaza wengi. Mshikaji wake Ramos, tayari ana kadi tano.

Javier Mascherano wa Barcelona ana faulo nane, tayari ana kadi ya njano na nyekundu.
Beki mwingine wa Barca, Gerard Pique  yeye ana faulo sabana kadi nne za njano!
Kitasa wa Atletico Madrid, Diego Godín ana faulo nane, kadi tatu za njano na patna wake Miranda ana faulo saba na kadi nne za njano.






0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic