Uongozi wa klabu ya Yanga imetuma majina 23 kwa ajili ya kikosi
chao kitakachoshiriki michuano ya Kombe la Shirikisho lakini imemtema kipa Juma
Kaseja.
Katika majina majina yaliyotumwa kwenye
makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf), hakuna jina la Kaseja.
Caf imeipanga Yanga kuanza na BDF ya
Botswana ambayo ni timu inayomilikiwa na jeshi la ulinzi la nchi hiyo.
Habari za uhakika kutoka Caf zimesema, Yanga
haijatuma jina la Kaseja na kusisitiza “hayumo”.
“Nimeangalia, hakuna jina la Kaseja. Je, una
swali jingine,” alihoji ofisa huyo wa Caf.
Wakati Kaseja anasajiliwa Yanga, uongozi wa
klabu hiyo ulitangaza kwamba zaidi umemsajili kwa ajili ya michuano ya kimataifa.
Lakini hivi karibuni aliingia kwenye mgogoro
na uongozi wa Yanga baada ya kudai amecheleweshewa malipo yake na Yanga ilikuwa
imevunja mkataba.
Kaseja aliipelekea Yanga barua akitishia
kufungua kesi mahakamani, halafu malipo yake yakafanyika.
Baada ya kulipwa, aliiandikia Yanga barua
nyingine akiiambia kwamba amepokea fedha zake na yuko tayari kuendelea
kuitumikia.
Hata hivyo Yanga haikuwahi kumjibu lolote,
zaidi ya kukaa kimya na Kaseja amekuwa kimya pia.
0 COMMENTS:
Post a Comment