Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia ambaye pia ni Mbunge wa Mtwara Vijijini
amejitolea kuisaidia timu ya Ndanda kuhakikisha inabaki Ligi Kuu Bara kwa
kujitolea fedha kiasi cha shilingi milioni 4.5 na posho za wachezaji kwa wiki.
Ndanda inashikilia mkia katika msimamo wa ligi
kuu kufuatia kuwa na pointi sita ikiwa imeshinda michezo miwili na kupoteza
michezo sita hivyo kujikuta katika wakati mgumu.
Mbunge huyo alitoa kiasi hicho kutokana na
kukabiliwa na ukata ambapo kiasi cha shilingi milioni 3 zitatumika kwa ajili ya
malazi na chakula huku milioni
1.5 kwa ajili ya kununulia vifaa mbalimbali vya michezo kwa wachezaji.
Msemaji wa
Ndanda, Idrisa Bandari alifunguka kuwa kiasi hicho cha fedha kitasaidia timu
hiyo kuwa katika kiwango kizuri ambapo waziri pia ameahidi kutoa posho ya
shilingi milioni 1.2 kwa wiki hadi msimu utakapoisha.
“Hii ni
changamoto kwetu kuhakikisha timu yetu inabaki katika ligi kwani hakuna
anayependa kuwa katika nafasi tuliyipo sisi,” alisema Bandari.
0 COMMENTS:
Post a Comment