Kocha mpya wa Simba, Goran Kuponovic amempendekeza Alphonce Gatera kuwa msaidizi wake.
Kutokana na uamuzi wake huo, Gatera na Selemani Matola ndiyo watakuwa makocha wasaidizi wa Simba.
"Kweli kocha amempendekeza Gatera kwa kuwa aliwahi kufanya naye kazi Polisi Rwanda.
"Tulimpa nafasi ya kuteua msaidizi. Matola anendelea kubaki pia kama kocha msaidizi. Mazungumzo na Gatera yameanza na tukikubaliana, atakuja Dar es Salaam ndani ya siku chache.
Gatera ni Myanrwanda aliyekulia nchini Burundi na walishirikiana vema na Kopunovic wakati akiinoa Polisi Rwanda.
0 COMMENTS:
Post a Comment