Aliyewahi kuwa mshambuliaji
wa Yanga Mganda, Hamisi Kiiza amefanikiwa kupata dili Uarabuni (Oman), katika
timu ya Fanja FC inayoshiriki ligi kuu nchini humo.
Mshambuliaji huyo aliachwa na
klabu yake kipindi cha dirisha dogo na nafasi yake kuchukuliwa na straika
Mliberia, Kpah Sean Sherman.
Kiiza ameichezea Yanga kwa
mafanikio makubwa tangu msimu wa mwaka 2012 na msimu uliopita alifanya vema
baada ya kuifungia mabao 12.
Kwa mujibu wa chanzo
ambacho ni ndugu wa kiungo huyo mshambuliaji huyo kwa sasa yuko katika
michakato ya kuelekea Uarabuni kwenda kusaini katika timu hiyo au nyingine ambayo
haikuitaja.
“Kiiza tulikuwa wote hapa
nchini, lakini kaondoka Jumatano ya wiki hii kurudi Uganda kisha atakwenda Uarabuni
kwa ajili ya kucheza soka, hapa nchini alifuata barua yake Yanga hivyo sijajua
kama amepewa au la,” alisema ndugu huyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment