Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm juzi
usiku alitumia dakika 90 kuzisoma timu za Simba na Mtibwa Sugar zilipokuwa uwanjani
zikiumana kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Hata hivyo, kasi kubwa ya wachezaji wa Mtibwa katika mchezo
huo uliokuwa na ushindani mkubwa, ilimtisha kocha huyo ambaye alifika uwanjani
hapo akiwa na ‘diary’ aliyokuwa ‘akinoti’ matukio yaliyokuwa yakiendelea ndani
ya uwanja.
Lakini pia mara kwa mara alikuwa akishauriana na msaidizi
wake, Charles Mkwasa, ambaye anaijua vema Mtibwa Sugar ambayo iliibuka na
ushindi wa bao 1-0 katika mchezo huo, kwa sasa timu hiyo ndiyo tishio kubwa kwa
Simba na Yanga kwenye Ligi Kuu Bara.
“Mtibwa Sugar wamecheza vizuri, wameonyesha kuwa si timu ya
kuidharau hivyo nimejifunza jambo kutoka kwao,” alisema Pluijm.
0 COMMENTS:
Post a Comment