KAGERA SUGAR... |
Michezo mitatu ya Ligi Kuu
Tanzania Bara inatarajiwa kupigwa leo Jumamosi katika viwanja tofauti, huku mchezo
mmoja ukimaliziwa kesho na mitatu ikiwekwa kiporo kutokana na timu zilizotakiwa
kucheza zinakabiliwa na Michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea Visiwani Zanzibar.
Kwenye Uwanja wa Mkwakwani,
Coastal Union itawakaribisha maafande wa JKT Ruvu ambao wana kumbukumbu ya kichapo cha bao 1-0 walichokipata
nyumbani msimu uliopita.
Maafande wa Ruvu Shooting
watapambana na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi. Huko Morogoro,
Polisi Moro wao watawakaribisha Stand United, Ndanda FC ambayo inashika mkia itakuwa
mgeni wa Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Katika raundi hiyo ya tisa
michezo kati ya Simba na Mgambo JKT, Azam na Mtibwa Sugar na Yanga na Mbeya
City imesogezwa mbele kutokaa na Klabu za Simba, Yanga, Azam na Mtibwa kuwa
kwenye Kombe la Mapinduzi.
0 COMMENTS:
Post a Comment