KOPUNOVIC AKIHOJIWA NA WAANDISHI WA GAZETI LA CHAMPIONI. |
Kocha mpya wa Simba, Goran
Kopunovic ametangaza mapemaa kwa wachezaji kuwa wajue yeye si mtu wa mzaha
katika suala la nidhamu.
Kopunovic amesema angependa
kufanya vizuri na anategemea ushirikiano wa karibu kwa wachezaji, benchi la
ufundi, uongozi na wanachama na mashabiki.
Lakini akasisitiza, suala
la nidhamu litakuwa namba moja na hatakuwa na mzaha.
“Hakuna kitu kinafanyika
kwa ufasaha katika maisha ya mwanadamu kama nidhamu haina uhakika.
“Hili ni sehemu ya misingi
bora ya kazi, itakuwa ni muhimu lipewe kipaumbele ni suala muhimu,” alisema.
Rais huyo wa Serbia ametua
kuchukua nafasi ya Patrick Phiri baada ya kuingoza Simba katika mechi nane za
Ligi Kuu Bara akiwa ameshinda moja, sare sita na kupoteza moja.
0 COMMENTS:
Post a Comment