January 1, 2015


Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm, amesema atatoa nafasi zaidi kwa ambao hawakuwa wakipata nafasi katika kikosi chake wacheze michuano ya Mapinduzi.


Pluijm raia wa Uholanzi, amesema anatoa nafasi ili kuweza kujua uwezo wa wachezaji wake wengine.

"Si lahisi kila mchezaji kupata nafasi ya kucheza kwenye ligi. Hii itaweka ugumu kidogo.

"Kikubwa hapa ni kuwapa nafasi wakati wa michuano ya Mapinduzi, itakuwa nafasi kwao kuonyesha walichonacho," alisema alipozungumza na SALEHJEMBE, mwaka jana ya Desemba 31.

Yanga inatarajia kuondoka leo kwenda Zanzibar ambako itashiriki michuano ya Mapinduzi.

Pluijm amerejea Yanga na kuchukua nafasi ya Marcio Maximo aliyechukua nafasi yake alipokwenda Uarabuni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic