January 1, 2015


Aliyekuwa Kocha  Mkuu wa Simba, Patrick Phiri amesema anapumzika kidogo, halafu ataondoka nchini kurejea kwao Zambia.


Phiri amezungumza na SALEHJEMBE na kusema sasa ana taarifa zote kuhusiana na kufutwa kwake kazi.

"Sasa kila kitu kiko wazi, lakini napumzika angalau siku moja, halafu nitaanza safari ya kwenda Zambia.

"Nawashukuru Wanasimba kwa sapoti, najua hii ni kazi. Acha nipumzike angalau siku moja mbili, nitaanza safari kurejea nyumbani," alisema Phiri.

Nafasi ya Mzambia huyo imechukuliwa na Mserbia, Goran Kopunovic ambaye tayari yuko jijini Dar.

Kopunovic amewahi kuinoa Polisi Rwanda lakini pia amefanya kazi nchini Vietnam.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic