Kocha mpya wa Simba, Goran Kopunovic
amesaini mkataba wa miezi sita.
Kocha huyo raia wa Serbia amekubaliana na
uongozi wa Simba kusaini mkataba huo hadi mwishoni mwa msimu.
“Kweli ndiyo makubaliano, baada ya hapo
litakuwa ni suala la kuangalia anachokifanya.
“Baada ya hapo, tutakuwa wote tumeona
tusaini mkataba zaidi au la,” alisema mmoja wa viongozi wa Simba.
Taarifa zinaeleza uongozi wa Simba
utamsafirisha Kopunovic hadi Zanzibar ambako atamaliza kila kitu.
“Kutakuwa na hafla maalum, hivyo naomba kwa
sasa utuache kwanza.”
0 COMMENTS:
Post a Comment