January 10, 2015


Na Zaidi Mwinshehe
Kocha Goran Kopunovic amesema kikosi chake kitaendelea kupambana kwa kila hali ili kishinde mechi yao ya fainali dhidi ya Mtibwa Sugar.


Fainali ya Kombe la Mapinduzi inapigwa Jumatatu kwenye Uwanja wa Amaan mjini hapa.

Kopunovic amesema anajua Mtibwa Sugar ni vinara wa Ligi Kuu Bara, lakini kikosi chake kinachojua ni kupamabana.

"Lazima tuwe na heshima na Mtibwa Sugar kwa kuwa ni moja ya timu kongwe na bora za Tanzania. Lakini kama nilivyosema mwanzo, tunataka kushinda.

"Tunaitumia michezo ya michuano ya Mapinduzi kujiandaa na Ligi Kuu Bara, lakini tunahitaji mafanikio.

"Hakuna asiyependa ushindi na hasa kutwaa ubingwa, hivyo tutapambana vilivyo," alisema.

Simba imetinga fainali ya Mapinduzi Cup baada yakuifunga Polisi Zanzibar bao 1-0.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic