January 10, 2015

MESSI (ALIYEPIGA MAGOTI) AKISHANGILIA NA WENZAKE BAADA YA KUFUNGA BAO PEKEE LA MECHI HIYO. 
Na Zaidi Mwinshehe, Zanzibar
Unaweza kusema sasa ni fainali ya Tanzania Bara ya Mapinduzi Cup baada ya Simba kuifunga Polisi Zanzibar bao 1-0.


Mechi imepigwa kwenye Uwanja wa Amaan hapa Zanzibar na kila timu ilionyesha imepania kushinda.

Lakini shujaa wa leo ni Ramadhani Singano ‘Messi’ aliyeifungia Simba bao pekee la mchezo huo.

Singano alipiga murua mkwaju wa faulo baada ya Danny Sserunguma alitekuwa akiwalamba chenga mabeki wa Polisi kufanyiwa madhambi.

Baada ya hapo, mechi hiyo ilikuwa ni vuta nikuvute na kila upande ukitaka kushinda.

Mwisho wa dakika 90, Simba imesonga fainali na sasa inakutana na Mtibwa Sugar.


Mtibwa na Simba zinakutana kwa mara ya pili katika michuano hii msimu huu baada ya wakata miwa hao kushinda bao 1-0 katika mechi ya kwanza dhidi ya Simba katika hatua ya makundi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic