Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic amesema
kikosi chake sasa ni suala la kazi mbele na hakutakuwa na sherehe yoyote
kufurahia ubingwa wa Kombe la Mapinduzi.
Akizungumza mjini Dar es Salaam, Kopunovic
amesema ushindi wa Kombe la Mapinduzi na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ndanda
FC katika Ligi Kuu Bara, hahitaji kuona watu wanasherekea.
“Kama unaulizia sherehe haitakuwepo, watu
kadhaa wameniuliza kuhusiana na hilo lakini hakuna sababu ya kufanya hivyo.
“Walijua baada ya kutoka Mtwara tutafanya
sherehe. Imeishapita, tumeshinda na sasa ni tunatengeneza timu kwa ajili ya
mechi nyingine.
“Kuifunga Ndanda hakikuwa kitu lahisi, wala
usidhani tumeshinda kwa kushitukiza au mimi sijui,” alisema Kopunovic raia wa
Serbia na kuongeza.
“Nimefundisha Rwanda kwa miaka mitatu, najua
mechi za ugenini zinavyokuwa ngumu. Najua unapokuwa na timu kubwa timu nyingine
zinapoikamia, hivyo tulijipanga.
“Kawaida ushindi mmoja unachangia watu
kukukamia zaidi, hivyo tunatakiwa kujipanga zaidi ndiyo maana sioni sababu ya
kuwa na sherehe.”
MSerbia huyo aliyechukua nafasi ya Patrick
Phiri kwa kushirkiana na msaidizi wake Selemani Matola wameiwezesha Simba
kubeba Kombe la Mapinduzi lililoshirikisha timu mbalimbali zikiwemo Yanga, Azam
FC, Mtibwa Sugar, Polisi Zanzibar, KMKM, Shaba, JKU na waliokuwa mabingwa
watetezi KCCA ya Uganda.
0 COMMENTS:
Post a Comment