Kiungo wa Manchester United, Anderson ameendelea kutanua licha ya kwamba amekuwa akichezea benchi.
Kiungo huyo raia wa Brazil amekuwa hana nafasi
katika kikosi cha Louis van Gaal.
Anderson ,26, ameanza katika kikosi cha kwanza
katika mechi sita kwa misimu mitatu.
Msimu huu amecheza dakika 20 tu, lakini
alionekana akitanua na rafiki yake wa kike katika jiji la Manchester. Raha jipe
mwenyewe, eeeh!
Kiungo huyo Mbrazili aliyejiunga na Man United akitokea FC Porto ya Ureno alikuwa akitanua na mrembo huyo mkali akiwa na gari lake aina ya Mercedes Benz lenye thamani ya pauni 200,000.










0 COMMENTS:
Post a Comment