BAADA ya michuano ya Kombe la Mapinduzi, sasa kazi
inarejea kwenye. Ligi Kuu Bara.
Michuano ya wiki ya Kombe la Mapinduzi mjini
Zanzibar tayari imepata mbabe wake, Simba na kombe liko jijini Dar es Salaam.
Vita ya vinara Mtibwa Sugar, Azam, Yanga na Simba
ambao wote wana viporo katika michuano ya ligi kuu, kutokana na kuwepo katika
ushiriki wa michuano ya Mapinduzi, lakini wikiendi hii- leo na kesho wanaendelea
kumsaka mwali wa Ligi Kuu Bara ambaye anahifadhiwa na Azam FC.
Kila upande una hofu, inajulikana kwa kuwa matokeo
hayana uhakika. Mechi za mwisho zinaonyesha Yanga na Azam waliambulia sare,
hali kadhalika Mtibwa Sugar wakati Simba walikutana na kichapo.
Yanga Vs Ruvu Shooting
Hata hivyo kwa jicho la harakaharaka, mechi za
wikiendi hii zimejawa hofu kwa timu zote zinazokutana, huku kubwa ikiwa ni ya
Yanga dhidi ya ‘vibonde’ wao wa msimu uliopita, Ruvu Shooting ambayo
ilinyweshwa mabao 7-0, ukiwa ni ushindi wa rekodi ya msimu. Pia vinara
wanaokabana kileleni, Mtibwa Sugar na JKT Ruvu, inatafsiriwa ni nguo kuchanika
kutokana na kila moja kutaka kubaki kileleni mwa msimamo.
Azam vs Stand United
(Kambarage)
Mabingwa watetezi, Azam wanaingia uwanjani leo
wakiwa na kumbukumbu ya kutofanya vema kwenye michuano ya Kombe la Mapunduzi na
kutupwa nje hatua ya robo fainali na Mtibwa Sugar.
Hata hivyo wikiendi hii ni kipindi cha kocah Joseph
Omog kurejesha imani kwa viongozi wake kwani Azam ni moja ya timu zenye kila
aina ya staa tena wa bei ghali lakini matokeo yake haijafanya vema kulinganisha
na thamani yao.
Ni mechi ya kufia uwanjani, kwani Stand ambao ni wanaingia na
hasira za kupoteza mchezo kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi walipochapwa na
JKT Ruvu, wikiendi iliopita.
Yanga vs Ruvu Shooting
(Taifa)
Moja ya mechi yenye hisia nyingi pande zote. Wakati
Yanga wakiingia kwa kujiahami kwa ushindi wa rekodi ya msimu wa mabao 7-0
waliovuna msimu uliopita, wanajeshi wa Ruvu Shooting wao wanasema ni kipindi
cha kulipiza kisasi hata kama si cha idadi ya mabao hayo.
Safu ya ushambuliaji
ya Yanga imezidi kuwa moto wa kuotea mbali hasa wakifanya maajabu kwenye
Mapunduzi, ambapo waliweka rekodi ya kufunga mabao tisa katika mechi tatu.
Hata
hivyo Ruvu wao wanasema ujio wa George Michael ‘Kifaru’ ambaye alikuwa ‘homa’
ya mastraika ni chachu ya kuwapunguza kasi akina Simon Msuva. Pia Ruvu wana
hasira za kuchapwa katika mchezo wa mwisho dhidi ya Mgambo Shooting, matokeo
yaliyowaweka nafasi ya tisa, hivyo kufungwa leo tena ina maana watakuwa na hali
ngumu zaidi.
Ndanda vs Simba
(Nangwanda Sijaona)
Itapigwa leo pia huko Kusini mwa nchi, lakini si
mechi yelele mama pande zote. Simba wanaingia wakiwa na furaha ya ubingwa wa
Mapinduzi, lakini pia hapohapo wakilizwa na matokeo mabovu kwenye ligi kuu.
Simba haihitaji kubeza mchezo huu kwa kujidanganya
na taji lao, badala yake akili yote ihamie kwenye matunda walio nayo ligi kuu.
Hata hivyo Ndanda wamekuwa wagumu zaidi kwa timu vigogo kwenye Uwanja huo,
ambapo mabingwa watetezi Azam walikubali kichapo cha bao 1-0 msimu huu.
Hivyo watauingia kwa tahadhari ya juu kuhusu ugumu
wa uwanja huo vinginevyo wanarudi mjini vichwa chini.
Kagera vs Mbeya City (CCM
Kirumba)
Nalo ni ‘goma’ la wiki hii. Timu zote zitakuwa
ugenini, unaweza kusema ni uwanja ‘neutral’ kutokana na uwanja wa nyumbani wa Kagera
Sugar, Kaitaba kuwa kwenye matengenezo hivyo mchezo kuhamishiwa mkoa jirani wa
CCM Kirumba, Mwanza.
Timu zote ‘zime-relax’ sana kutokana na kutokuwa na
mechi kufuatia ratiba ya Mapinduzi. Zina rekodi sawa kwani msimu uliopita
zilitoshana nguvu mechi zote mbili.
Lakini Mbeya City wanajua Kagera Sugar wako ‘on
fire’ baada ya kutoka kuitwanga Simba kwa bao 1-0 katika mechi ya ugenini.
Hivyo bado Kirumba haiwezi kuwa ugenini sana kwao na vijana wa Juma Mwambusi
wanatakiwa kuwa makini kweli.
Mgambo Vs Prisons
Uwanja wa Mkwakwani hautapumzika kwa siku mbili
mfululizo wakati Mgambo ikiwa mwenyeji wa Prisons katika mechi itayotarajiwa
kuwa ngumu na yenye kutumia nguvu nyingi sana kwa kuwa kila upande wako fiti
kweli.
Kesho, kutakuwa na kazi nyingine wakati Wagosi wa
kaya Coastal Union wakiwakaribisha Polisi Moro, moja ya timu inayocheza soka
safi na la kitabuni.
Coastal licha ya kutokuwa katika tatu bora katika
msimamo ni moja ya timu yenye kikosi chenye wachezaji wazuri wa kigeni kutoka
katika nchi za Nigeria, Uganda na Kenya.
Lakini hiyo haiwezi kuwa sababu ya
kuisimamisha Polisi kabla ya dakika 90 ambazo ndiyo zitatoa jibu na lazima kazi
ifanyike.
JKT Ruvu Vs Mtibwa (Chamazi Complex)
Pia kesho kutakuwa na mechi nyingine ‘ngangari’
wakati vinara wa ligi hiyo, Mtibwa Sugar watakapokuwa wakitafuta pointi zaidi
safari hii wakiwa ugenini dhidi ya JKT Ruvu.
Mechi itapigwa kwenye Uwanja wa Uwanja wa Azam
Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam. Itakuwa moja ya mechi ngumu na Mtibwa
wanapaswa kuwa macho kweli maana wanajeshi hao sasa hawatabiriki.








0 COMMENTS:
Post a Comment