Kocha Msaidizi ya Simba, Selemani
Matola, juzi usiku alijikuta akidondosha machozi baada ya timu hiyo kuchezea
kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Amaan kisiwani
hapa.
Kutokana na hali hiyo, Matola
aliwashushia lawama wachezaji wa kimataifa timu hiyo kutoka Uganda ambao
hawakuambatana na kikosi hicho visiwani hapa kwa ajili kushiriki Mashindano ya
Mapinduzi yalioanza juzi Alhamisi.
Waganda hao ni Emmanuel Okwi, Simon
Sserunkuma, Juuko Mrushid na Joseph Owino ambao kwa pamoja hawakuweza
kuambatana na kikosi hicho kutokana wote kudaiwa kuwa kwao nchini Uganda.
Matola amesema kuwa
kikosi chake kimeshindwa kuibuka na ushindi katika mchezo huo kutokana na
kukosekana kwa nyota hao.
“Kukosekana kwa wachezaji wa kimataifa
ndiyo hasa kumesababisha tupate matokeo haya kwa sababu nimelazimika kuchezesha
wachezaji wasiokuwa na uzoefu wa mashindano, hivyo nadhani jambo hili viongozi
watakuwa wameliona na watalifanyia kazi,” alisema Matola.
0 COMMENTS:
Post a Comment