Baada ya kipa, Juma Kaseja kuachwa kwenye kikosi cha Yanga kitakachoshiriki michuano ya kimataifa kocha wa makipa wa timu hiyo, Juma Pondamali ‘Mensah’ amesema
kukosekana kwa nguli huyo siyo tatizo kwani timu bado ina makipa wazoefu na
wenye uwezo.
Yanga
imepangwa kuanzia nyumbani katika michuano hiyo kwa kucheza na timu ya jeshi ya
Botswana, BDF IX kati ya Februali 13 hadi 15 mwaka huu na tayari imetuma majina
23 kwenda Caf, huku Kaseja ‘akimwagwa’.
Akizungumza
na Championi Jumamosi, Pondamali alisema kukosekana kwa kipa huyo siyo tatizo
kwa kuwa waliopo wana uzoefu, ndiyo maana hata Deogratius Munishi ‘Dida’
anaidakia timu ya taifa, Taifa Stars.
“Kaseja
ni kipa mzuri mwenye uzoefu katika soka la kimataifa, hilo silipingi, lakini
kukosekana kwake siyo ishu kwani makipa waliopo wana uzoefu na michuano hiyo.
“Binafsi
sijui kama jina lake limetumwa Caf au la, lakini kama kweli halijatumwa bado
Yanga ina nafasi ya kufanya vizuri kulingana na aina ya makipa tulionao,”
alisema Pondamali.
0 COMMENTS:
Post a Comment