January 10, 2015


OKWI (KUSHOTO) AKIWA KWENYE UWANJA WA AMAAN HIVI PUNDE...
Na Saad Mwinshehe, Zanzibar
Wakati Simba inapambana kuwania kusonga fainali dhidi ya Polisi Zanzibar, kiungo Emmanuel Okwi naye yuko kwenye Uwanja wa Amaan, hapa Zanzibar.

Okwi alikuwa gumzo kwa madai alichelewa kurejea ingawa hali halisi ilikuwa hivi; alitakiwa kurejea jana Ijumaa kwa mujibu wa ruhusa aliyopewa, maana yake hakuchelewa.

Okwi yuko kwenye benchi la Simba lakini inaonyesha hatacheza mechi ya leo kwa kuwa hajafanya mazoezi hata siku moja chini ya Kocha Goran Kopunovic.

Okwi alionekana akizunguka uwanjani na mratibu wa Simba na baadaye kwenda kukaa kwenye benchi la Simba.

Sasa mechi inaendelea na Simba inaongoza kwa bao moja lililofungwa na Ramadhani Singano kwa faulo baada ya Danny Sserunkuma kuangushwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic