Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema anapenda kikosi kinachocheza kwa kasi na kujilinda kwa kushambulia.
Pluijm raia wa Uholanzi amesema hapendi kikosi kinachocheza soka la kubaki langoni kwa ajili ya kujihami.
Katika mahojiano maalum na SALEHJEMBE kutoka Zanzibar, Pluijm amesema unaposhambulia, kitaalamu unakuwa unajilinda.
"Unaposhambulia maana yake una mpira, adui hawezi kushambulia wakati hana mpira. Maana yake unalinda wakati huo huku ukitekeleza lengo la ulinzi.
"Sioni kama sawa kukaa nyuma na kusubiri adui aje na kukushambulia. Soka lina mambo mengi na ikitokea hivyo ujue tuna jambo tunalitaka.
"Kuna mambo kadhaa mimi na Charles (Boniface Mkwasa) tunajitahidi kurekebisha," alisema Pluijm.
Yanga inashiriki michuano ya Mapinduzi mjini Zanzibar na tayari imecheza mechi moja na kushinda kwa mabao 4-0.
0 COMMENTS:
Post a Comment