February 24, 2015

HOTELI WALIYOFIKIA SIMBA...
Ndani ya Simba kunafukuta! Inawezekana ikawa mapema sana kwa viongozi kulianika hilo.
Inaonekana ndani ya viongozi wako wenye furaha kikosi chao kupoteza na wengine wana majonzi.



Lakini mjadala mkubwa wa Simba kupoteza bao 1-0 dhidi ya Stand United unaonekana kwenda kusipo sahihi.

Nilizungumza na mdau mmoja wa Simba ambaye ni kati ya viongozi wa kamati ua utendaji, yeye alinieleza kinachomuuma ni Simba kupoteza dhidi ya Stand United.

Anaamini Stand United si timu ya kuifunga Simba na moja kwa moja akatupa lawama kwa viongozi ambao waliambatana na timu Shinyanga.

Kati ya walioambatana na timu Shinyanga ni Musley Al Rawah, Kassim Dewji, Hans Poppe na Rais Evans Aveva.

Maana yake Simba ilikuwa kamili Shinyanga, Stand wakaonyesha wana uwezo na kuifunga bao 1-0.
Kama Simba wataamua kufanya mjadala wa kufungwa, iko haja ya kuufanya bila ya kutanguliza dharau kwa Stand.

Kwani Stand si timu inayoweza kuifunga Simba? Kwa nini wakati ni timu ya Ligi Kuu Baea? Usisahau, Simba ilitoka sare ya bao 1-1 katika mzunguko wa kwanza dhidi ya timu hiyo tena kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Ukiangalia hata mazingira waliyoishi Simba mjini Kahama kabla ya kwenda Shinyanga ni ya kuvutia.
Wakati mwingine unaweza kushindwa kuwalaumu viongozi hao kwa kuwa walitoa kila kitu kwa timu hiyo.

Wachezaji pia wanaweza kusema walijitahidi kwa kuwa, kupitia runinga tuliona soka la kuvutia.
Maana yake, Simba wanapaswa kujadili kilichowapoteza na kujipanga kwa mchi ijayo na si dharau kwa Stand ndiyo iwe mjadala.
 
Umeona Azam FC ikitoka sare ya bila kufunga dhidi ya Prisons kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar.

Usisahau, Prisons imetoka kufungwa mabao 3-0 dhidi ya Yanga tena nyumbani kwao. Azam FC walikuwa wametoka kwenye suluhu dhidi ya Ruvu Shooting, wakasema Uwanja wa Mabatini ni mbaya sana.
Waliporudi Chamazi, wakakutana na sare nyingine tena. Hawana la kusingizia wamekaa kimya, huo ndiyo mpira.

Hivyo Simba wakiamua kuweka mjadala mezani, iko haja ya kuangalia sababu za msingi zilizowaangusha badala kutanguliza ukubwa au udogo wa timu waliyocheza nayo kama mjadala sahihi!






0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic