February 11, 2015


Mtibwa Sugar imezidi kuonja joto ya jiwe katika jiji la Dar es Salaam, safari hii ikikumbana na kipigo cha aibu cha mabao 5-2 kutoka kwa Azam FC.


Katika mechi hiyo kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar, Mtibwa ilipata kipigo hicho cha pili mfululizo baada ya kuwa imelala kwa mabao 2-0 dhidi ya Yanga katika mechi iliyopita.

Wachezaji wawili wa zamani wa Yanga, Didier Kavumbagu na Frank Domayo ndiyo waliokuwa mashujaa baada ya kila mmoja kufunga mabao mawili.
Bao la tano lilifungwa na raia wa Ivory Coast, Kipre Tchetche.

Hadi mapumziko Mtibwa Sugar ilikuwa nyumba ka mabao 3-1, mawili yakifungwa na Kavumbagu, moja Domayo na wao Mtibwa wakiwa wamepata bao kupitia Salum Mpakala.


Kipindi cha kwanza ndiyo kilikuwa kigumu zaidi kwa Mtibwa waliomaliza mzunguko wa kwanza wakiwa wanaongoza ligi kuu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic