Azam FC imeng’oka katika michuano ya Kombe
la Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa El
Merreikh.
Azam FC ilishinda kwa mabao 2-0 jijini Dar,
hivyo kufanya ing’oke kwa jumla ya mabao 3-2.
Katika mechi iliyochezwa leo jijini
Khartoum, Sudan, Azam FC ilianza kukubali bao katika dakika ya 11 mfungaji
akiwa Coffie.
Bao hilo lilidumu hadi kipindi cha kwanza na
ilikuwa ni kuhakikisha Azam wanakomaa hadi mwisho, lakini ikashindikana.
Merreikh ilipata mkwaju wa penalti kutokana
na faulo ya Serge Wawa, lakini ikakosa.
Baada ya hapo, mambo yalionekana kuwa magumu
kwa Azam FC katika kipindi cha pili ambayo ilitaka kujilinda zaidi.
Dofr akaifungia Merreikh bao la pili katika
dakika ya 85, Mkenya Allan Wanga aliyeingia kipindi cha pili, akafunga bao la
tatu katika dakika ya 90 na kuimaliza Azam.
0 COMMENTS:
Post a Comment