February 22, 2015


Mbunge wa Mbeya mjini kupitia Chadema, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu, leo alimkaribisha mwenyekiti wa chama hicho kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.


Sugu alimkaribisha kushuhudia timu anayoishabikia kutoka jimbo lake ya Mbeya City wakati ikicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Yanga.

Ilikuwa mechi ya Ligi Kuu Bara na Mbowe alikuwa kati ya mashabiki walioshuhudia Mbeya City ikitandikwa mabao 3-1 licha ya kuwa nyumbani.

Sugu aliungana na mashabiki jukwaani kama ilivyo kawaida yake lakini haikumzuia kuona mabao matatu ya Simon Msuva, Mrisho Ngassa na Mrundi Amissi Tambwe yakiididimiza timu yake nyumbani, tena mbele ya mgeni wake.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic