February 22, 2015


Ushindi una raha yake bana! Maana Mrisho Ngassa leo alikuwa haishi vituko wakati Yanga ilipoitwanga Mbeya City kwa mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Ngassa aliyekuwa mmoja wa wafungaji, mara baada ya kufunga bao lililokuwa na pili, alikimbia hadi nje ya 'pitch' na kumfuata swahiba wake Jerry Tegete.

Alipomfikia, Ngassa alionyesha kama anataka kumpiga vile, naye Tegete aliyekuwa amevaa kandambili za Simba 'za Simba', alionyesha kama anataka kujibu mapigo.

Lakini Simon Msuva alikuwa kama vile 'anaamua', basi 'ugomvi' ukaisha. Eh!


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic