February 21, 2015


Kiungo wa Yanga, Andrey Coutinho amesema ana uhakika ataendelea kufunga na kusababisha mabao katika kila mechi atakayocheza.



Katika mechi iliyopita dhidi ya Prisons, Countinho ambaye ni mchezaji pekee anayetumia mguu wa kushoto wa asili, alifunga bao moja huku mawili yakifungwa na Simon Msuva.

Coutinho, amesema sasa anaanza kuzoea mazingira ya soka nchini kwa kuwa awali amekuwa akipata shida pia akapongeza ushirikiano anaoupata kutoka kwa wachezaji wenzake.

"Mazingira hayalingani na Brazil, lakini ilikuwa shida kidogo kuzoea. Hata sasa bado najifunza lakini angalau naweza kucheza kwa utulivu.

"Mambo yataenda vizuri zaidi, kwangu ninafurahi nikifunga au kusababisha bao. Najua naweza kufanya kazi zote," alisema.

Coutinho yuko Mbeya na kikosi cha Yanga ambacho kesho kina kazi ya kuwavaa Mbeya City waliopania kushinda.

Kiungo huyo alijiunga na Yanga wakati kocha akiwa Marcio Maximo, raia wa Brazil pia. Baadaye Maximo alitimuliwa na uongozi baada ya kuonekana mwenendo haukuwa mzuri.

Tayari Yanga imecheza mechi dhidi ya Priosns na kushinda kwa mabao 3-0 mjini humo. Lakini itakuwa na kazi ngumu dhidi ya Mbeya City.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic