February 1, 2015




Kama ulikuwa unashangaa refa wa Toto dhidi ya Polisi Tabora akikimbizwa kama mwizi, sasa zamu ya kushangaa michuano ya Kombe la Mataifa Afrika.

Mwamuzi wa mchezo kati ya wenyeji Equatorial Guinea dhidi ya vigogo Tunisia aliishia kukimbizwa na wachezaji wa Tunisia wakitaka kumdunda.


Wachezaji hao walisai mwamuzi huyo alitoa penalti kwa wenyeji na haikuwa penalti na wenyeji hao wakafunga na kusababisha mechi iongezwe dakika 30 na mwisho wakaishia kushinda 2-1 na kuwatoa Tunisia.

Mara baada ya mechi, mwamuzi huyo alikuwa katika wakati mgumu huku wachezaji wa Tunisia wenye jazba kama nyati wakimkimbiza.


Polisi na walinzi wa uwanjani hapo walilazimika kufanya kazi ya ziada kumuokoa. Ehh!









0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic