February 1, 2015


Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema mechi ya leo dhidi ya Ndanda ni sahihi kwao kujirekebisha na kuyafanyia kazi waliyojifunza kwa zaidi ya siku 7.


Yanga inaikaribisha Ndanda FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, leo.

Pluijm raia wa Uholanzi amesema ni wakati mwafaka kuyafanyia kazi mambo walioyokosea katika mechi iliyopita.

"Ushindi ndiyo jambo muhimu, lakini hatuwezi kushinda kama hatujayafanyia marekebisho matatizo yetu.

"Ninaamini wachezaji watafanya hivyo na itakuwa njia ya kuendelea kufanya vizuri zaidi," alisema.

Pluijm amesema anaamini ana kikosi kizuri kinachoweza kuifumua Ndanda lakini lazima nafasi zitakazopatikana zitumiwe kwa asilimia angalau 70.

Yanga imekuwa ikiongoza kwa kutengeneza nafasi nyingi, pia kupoteza nyingi katika Ligi Kuu Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic