February 22, 2015


Kama walivyofanya Mbeya City, mashabiki wa Stand United wamekesha wakiulinda Uwanja wa Kambarage ili Simba wasichimbie 'ndumba'.



Baadhi ya mashabiki wa Stand United wamekuwa uwanjani hapo usiku wote wakihakikisha hakuna mtu anayeingia ndani ya uwanja huo uliopo mjini Shinyanga.

Simba inaivaa Stand kwenye uwanja huo ikiwa ni mechi ya marudiano ya Ligi Kuu Bara baada ya sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar katika mzunguko wa kwanza.

Tayari wachezaji wa Stand wameporwa timu zao na viongozi kwa hofu ya hujuma.

Mashabiki wa Mbeya City bao wamekesha wakilinda uwanja wa Sokoine ili kuzuia mashabiki wa Yanga kuingia usiku na "kufanya mambo yao".

Hivi karibuni, mashabiki wa Coastal Union na wanachama walikesha uwanjani wakilinda Mkwakwani kwa hofu hiyohiyo ya ushirikina.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic