February 4, 2015

KOPUNOVIC AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA CHAMPIONI, MARTHA MBOMA, MOHAMMED NA OMARY MDOSE...
 Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic amesema amekuwa akishirikiana vizuri na vyombo vya habari tokea ametua nchini.

Lakini akasema waandishi wa Gazeti la Michezo la Championi, ndiyo wamekuwa wakimbana zaidi kila wakati.
"Hauwezi kuweka kila kitu cha timu kwenye vyombo vya habari, lakini kuna mambo ambayo waandishi wanastahili kuyajua, lazima uwape ushirikiano.

"Mfano rafiki zangu wa Championi hawakosi mazoezi, nawaona pia kila baada ya mechi. Wana maswali mengi sana (kicheko).

"Lakini ni sehemu ya kazi na tumekuwa tukiendelea kushirikiana na ikiwezekana kurekebishana," alisema Kopunovic raia wa Serbia.

Kocha huyo ametua kuinoa Simba akitokea Don Long Tam ya Vietnam lakini aliwahi kufanya kazi barani Afrika katika kikosi cha Polisi Rwanda alichokifundisha kwa takribani misimu mitatu na usheee.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic