Kampuni ya Multichoice leo imezindua rasmi king’amuzi chake cha
HDZAPA chenye ubora zaidi katika picha zake na ‘applicationi’ ya DStv now maalumu kwa ajili ya simu, laptop,
tablets na hii ni kwa wateja pekee wa ving’amuzi vya Dstv.
King’amuzi hicho chenye ubora na uwezo wa hali ya juu na mvuta katika picha zake kwa kiwango cha
juu cha sauti ‘dolby digital5.1 .
| SHELUKINDO... |
Akizungumza na katika
uzinduzi huo, Meneja Uendeshaji wa Dstv, Ronald Baraka Shelukindo alisema king’amuzi
hicho na huduma hiyo itakuwa ya kipekee kwa watanzania na watapata fursa
kuangali chaneli tofauti huku picha zikiwa ubora wa hali ya juu.
| FURAHA NA BARBRA |
“ Tumezindua king’amuzi chetu kipya cha Dstv HDZAPA ambayo itakuwa na picha zenye ubora wa hali
ya juu kuliko ving’amuzi vya awali
pamoja na huduma ya Dstv Now ambayo itamrahisishia mteja wetu kuweza
kuangalia chaneli na vipindi
tofauti tofauti kupitia simu ya mkononi, tablets, laptop kama atakuwa ni mteja
halali lakini.
“Na sasa vipo katika
nchini nzima kwa mawakala wetu kwa wateja wapya wa Dstv watanunua kwa
shilingi 99000 na wale wazamani
ukienda na king’amuzi cha awali utalipia kiasi cha shilingi 39000 tu,”alisema
Shelukindo.







0 COMMENTS:
Post a Comment