MPIRA UMEKWISHA:
Dk 90, mwamuzi anampa Joshua kadi ya njano
kwa kucheza kindava.
Dk 88 Coastal wanafanya shambulizi lakini
Oscar Joshua anafanya kazi ya ziada na kuokoa.
Dk 85 Mohamed Mtindi anampiga Twite buti la
kichwa, anapewa kadi ya njano.
Dk 83 Yanga wanamtoa Tambwe ambaye anatoka
akiwa amebebwa kwenye machela na nafasi yake inachukuliwa na Danny Mrwanda
Dk 79 yeye na Barthez, anapaisha juuuuu
Dk 71 Said Juma 'Makapu' analambwa kadi ya njano kutokana na kuchza kindavaDk 65 Yanga wanamtoa Coutinho na nafasi yake inachukuliwa na Hussein Javu
Dk 63, Tambwe anapiga shuti kali lakini unatoka nje
Dk 60, Twite anapiga shuti kali la faulo lakini anashindwa kulenga lango.
Dk 58 Tumba Sued analambwa kadi ya njano kwa kumfanyia madhambi Sherman
Dk 52 Tumba anafunga lakini hata hivyo alikuwa ameisaotea...
Dk 49 Itubu Imbem anaingia ndani ya eneo la hatari la Yanga baada ya pasi nzuri ya Humud, lakini Tambwe aliyekuwa amerudi nyuma anaokoa
Dk 46 Sherman anaingia kwenye lango la Coastal na kujaribu kupiga lakini anazuiwa
MAPUMZIKODk 44, Sherman anapiga kichwa safi lakini mpira unatoka nje
Dk 38 pasi nzuri ya Humud inaingia kwenye lango la Yanga lakini Barthez anafanya kazi ya ziada kuokoa.
Dk 36, Coutinho anapiga shuti kali linatoka juu kidogo ya lango la Coastal
Dk 31 Tumba anapiga shuti kali lakini linaokolewa na mabeki wa Yanga
Dk 23, Rama Salim anapiga mpira wa adhabu unaokolewa na kuwa kona isiyo na matunda
Dk 18, vurugu zinatawala uwanjani, mashabiki wakipigana mawe na polisi wanalazimika kuingilia.
Dk 15 krosi nzuri ya Msuva, lakini Kado anaokoa vizuri na kusababisha kona mbili ambazo hazizai matunda.
GOOOOOOOOO Dk 11, Cannavaro anaifungia Yanga bao la kwanza kwa kichwa baada ya kuuwahi mpira wa kurusha wa Twite.
Dk 7, Coutinho anapiga mpira wa faulo lakini Shabani Kado anafanya kazi ya ziada kuundosha.
Dk 4, Abdulhalim Humud anapiga mpira wa
faulo kwenye lango la Yanga na kuzaa shambulizi kali lakini shuti la Rama Salim
linaokolewa na Barthez.
Dk ya kwanza, Coastal ndiyo wameanza kufika kwenye lango la Yanga, lakini baadaye nao wanafika lakini si mashambulizi makubwa kwa kuwa yanadakwa kilaini na makipa.







0 COMMENTS:
Post a Comment