February 23, 2015


Straika Charlie Austin wa Queens Park Rangers amemtolea uvivu kiungo mkongwe wa timu hiyo Joey Barton kwamba aliwaponza.


Barton alitolewa kwa kadi nyekundu katika mechi dhidi ya Hull City baada ya kumpiga kwenye korodani kiungo Tom Huddlestone.
 
AUSTIN AKISHANGILIA BAADA YA KUFUNGA BAO LA KUONGOZA KABLA WAO HAWAJAFUNGWA MENGINE MAWILI...
Barton alifanya kitendo hicho ikiwa ni baada ya kumchezea madhambi beki Alex Bruce.

QPR ilipoteza mechi hiyo baada ya kuwa imetangulia kwa bao la Austin ambaye baada ya kufunga aliigiza kama mlemavu.

Barton anaaminika mmoja wa wachezaji wakorofi zaidi katika Ligi Kuu England.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic