February 24, 2015

KIKOSI CHA YANGA KILICHOITWANGA BDF BAO MBILI MTUNGI.

Kikosi cha Yanga kinatarajia kuondoka nchini kesho kwenda Botswana kwa ajili ya kuwavaa BDF XI katika mechi ya Kombe la Shirikisho.


Yanga itaondoka nchini ikiwa na kikosi cha wachezaji 20 pamoja na memba wa benchi la ufundi pamoja na baadhi ya viongozi.

Katika mechi ya kwanza, Yanga ikiwa nyumbani ilishinda kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Mrundi, Amissi Tambwe.

Safari hiyo ya Yanga kwenda Botswana ni kumalizia mechi hiyo ya pili.

Kabla ya safari hiyo, Yanga ikiongozwa na Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm ilishinda mechi tatu ikianza kwa kuitwanga BDF XI kabla ya kuhamia kwenye ligi.


Katika mechi za Ligi Kuu Bara, Yanga ilianza kwa kuitungua Prisons kwa mabao 2-0, halafu ikageuka na kuichapa Mbeya City kwa mabao 3-1 kuthibitisha kuwa haikubahatisha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic