February 24, 2015


Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm ameamua kuwapumzisha wachezaji wake.


Pluijm amekipumzisha kikosi chake akisema mechi tatu ndani ya siku naye ni moja ya kazi ngumu.

“Kweli, leo nimeahirisha kufanya mazoezi kwa kuwa wachezaji lazima wapumzike.

“Ndani ya siku nane wamcheza mechi tatu, zote ni ngumu. Nimeona kabla ya safari, lazima wawe na nafasi ya kupumzika,” alisema Pluijm.

Yanga imecheza mechi tatu mfululizo na kushinda zote ikiwemo moja ya michuano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya DBF XI.

Katika mechi dhidi ya BDF XI, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 kabla ya kusafiri hadi jijini Mbeya ilikocheza mechi mbili.


Katika mechi hizo za Ligi Kuu Bara, Yanga ilianza kwa kuitungua Prisons kwa mabao 2-0, halafu ikageuka na kuichapa Mbeya City kwa mabao 3-1 kuthibitisha kuwa haikubahatisha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic