Timu ya Taifa ya Tanzania ya soka la
ufukweni (Beach Soccer) inatarajiwa kuodoka siku ya alhamisi kuelekea jijini
Cairo nchini Misri kwa ajili ya mchezo wa marudiano kuwania kufuzu kwa fainali
za Mataifa Afrika kwa soka la ufukweni utakaofanyika siku ya jumapili.
Tanzania inapaswa kupata ushindi katika
mchezo wa marudiano dhidi ya Misri utakaofanyika siku ya jumapili jijini Cairo
ili kufuzu kwa fainali za soka la ufukweni barani Afrika zitakazofanyika visiwa
vya Shelisheli kufuatia kupoteza mchezo wake awali uliofanyika Escape 1 jijini
Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
Msafara wa timu ya Beach Soccer
utakaoondoka na shirika la ndege la Ethiopia, utaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya
Utendaji Ahmed Msafiri Mgoyi, kocha mkuu John Mwansasu, kocha msaidizi Ali
Sheikh Alhashby, meneja Deogratius Baltazar na daktari wa timu Dr Leonidas
Rugambwa.
Wachezaji ni Rajabu Chana Kipango, Ahmed
Rajab Juma, Roland Revocatus Kessy, Samwel Sarungi Opanga, Feisal Mohamed Ussi,
Mohamed Makame Silima, Mwalimu Akida Hamad, Juma Sultan Ibrahim, Kashiru Salum
Said na Ally Rabby Abdallah.







0 COMMENTS:
Post a Comment