Msafara wa watu 25 wa timu ya Taifa ya
Tanzania ya Wanawake (Twiga Stars), unatarajiwa kuondoka nchini siku ya ijumaa
kuelekea nchini Zambia kwa ajili ya mchezo wake wa kwanza dhidi ya timu ya
Taifa ya Wanawake ya Zambia siku ya jumapili.
Twiga Stars inaanzia hatua ya pili katika
kuwania kufuzu kwa Fainali za Afrika kwa Wanawake baada ya kuwa katika nafasi
za juu kwa viwango barani Afrika, na endapo itafanikiwa kuwaondoa Wazambia
itafuzu moja kwa moja kwa fainali hizo.
Msafara utaongozwa na Blassy Kiondo
(Mjumbe wa Kamati ya Utendaji), Beatrice Mgaya (kiongozi msaidizi), Rogasin
Kaijage (kocha mkuu), Nasra Juma (kocha msaidizi), Furaha Francis (Meneja),
Christine Luambano (Daktari) na Mwanahamis Abdallah (Mtunza vifaa).
Wachezaji watakokweda Zambia ni Asha
Rashid, Mwajuma Abdallah, Mwanahamis Omar, Donisi Minja, Amina Bilal, Fatuma
Bashiri, Esther Chabruma, Shelda Mafuru, Maimuna Kaimu, Najiat Abbas, Stumai
Abdalla, Fauma Issa, Thereza Yona, Fatuma Hassan, Fatuma Omary, Sophia
Mwasikili, Fatuma Khatibu na Etoe Mlenzi.








0 COMMENTS:
Post a Comment