Katika kuhakikisha
timu yao inafanya mazoezi kwenye hali tulivu na salama, Yanga wamejificha kwenye
eneo lenye msitu mkubwa huku kukiwa na siafu wengi.
Yanga wanajiwinda na
mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,
Jumapili ijayo.
Yanga yenyewe
iliyoweka kambi yake kwenye hoteli moja Bagamoyo huko Pwani, inatoka umbali
mrefu kuufuata uwanja ambao umezungukwa na pori kubwa huku kukiwa na milio ya
ndege tu.
Kufika kwenye uwanja
huo ni shughuli pevu kwani hakuna gari lolote linaloweza kufika huko zaidi ya
pikipiki, hali iliyosababisha kuwa na mashabiki wachache sana.
Katika mazoezi ya
jana asubuhi yaliyofanyika kwenye uwanja huo, watazamaji wakubwa waliokuwa
wakifuatilia mazoezi hayo yaliyoongozwa na kocha msaidizi Charles Mkwasa ni
wanafunzi pekee wa chuo hicho wanaofikia 15.
Kubwa kuliko yote,
uwanja huo umezungukwa na wadudu aina ya siafu ambao kama ukisimama au kukaa,
lazima watakutambaa kutokana na mazingira ya msitu uliouzunguka uwanja huo.
0 COMMENTS:
Post a Comment