March 4, 2015


Huku homa ya pambano la watani wa jadi, Simba na Yanga ikizidi kupanda, imefahamika kuwa mchungaji, Ammy Sentimeya wa kanisa moja huko Temeke ndiye atakuwa kamisaa wa mchezo huo wenye mvuto wa aina yake.


Mechi ya Simba na Yanga imekuwa ikivuta hisia za mashabiki kwa nchi nzima na mara nyingi zimekuwa na changamoto nyingi baada ya kumalizika.

Taarifa za uhakika kutoka kwenye kamati ya waamuzi, zinasema kuwa Martin Saanya ambaye mashabiki wa Yanga haziivi, ndiye amepewa ‘rungu’ katika kesi hiyo, kama mwamuzi wa kati akisaidiwa na Idd Lila wa Dar es Salaam pamoja na Florentina Zabrone, kutoka Dodoma, wakati Israel Nkongo akisimama kama mwamuzi wa mezani.

Saanya bado mashabiki wa Yanga hawana imani naye tangu ashutumiwe kuwanyonga katika mchezo na Coastal Union msimu wa 2012/13 , baada ya kuipa Coastal penalti dakika za mwisho kabisa, hali iliyosababisha vurugu kubwa na uharibifu wa mali.

““Kamisaa wa mchezo huo ni mchungaji, sijapata jina la kanisa lake lakini ni huko Temeke.


“Kwa kazi yake hakika tunaamini atakuwa mtu sahihi kwetu kutuandalia ripoti yenye haki na ambayo haiwezi kuwa na uchakachuaji,” kilisema chanzo cha ndani kutoka kwenye kamati ya waamuzi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic