March 6, 2015


Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Andrey Coutinho, juzi Jumatano alishindwa kujizuia na kujikuta akimwaga chozi mara baada ya kupewa taarifa ya kuikosa mechi dhidi ya Simba.


Mbrazili huyo alifanyiwa vipimo kwenye Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam na baada ya hapo ndipo akapewa taarifa hizo ambapo anasumbuliwa na maumivu ya goti aliyopata wakati timu hiyo ilipovaa na Mbeya City katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Prisons.

Coutinho alisema kuwa bora angekosa mechi zote lakini siyo dhidi ya Simba yenye upinzani mkubwa.

“Ninaumia sana kuikosa mechi dhidi ya Simba, kauli iliyotolewa na madaktari leo (Jumatano) mara baada ya kufanyiwa vipimo imenifanya nikose furaha,” alisema Coutinho.

Aidha, Coutinho aliongeza kuwa, anaamini kikosi chake kipo fiti na wachezaji wenzake lazima watawafunga Simba kutokana na jinsi walivyo fiti kwa sasa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic